Kocha wa klabu ya Lokomotiv Moscow Markus Gisdol mwenye asili ya Ujerumani amevunja mkataba na klabu hiyo kutoka na kupinga uvamizi uliofanywa na nchi ya Urusi kwenye taifa la Ukraine.
Klabu ya Lokomotiv Moscow ilitoa waraka mfupi uliosimeka “Markus Gisdol ameondolewa kwenye nafasi yake ya kocha mkuu wa klabu” baada ya kuwa kocha kwa miezi minne kwenye klabu hiyo aliliambia German tabloid Bild, alikuwa anaunga mkono kupinga kwa kukataa kufanya kazi kwenye nchi ambayo kingozi wake anahusika na uchokozi wa kivita katikati ya bara la ulaya.
“siwezi kusimamia mazoezi jijini moscow, makocha na wachezaji wanapaswa kusimamia taaluma na kilomita kadhaa kwenye mipaka kuna watu wanateseka kwa sababu ya vita iliyoanzishwa na kiongozi wa nchi kwa matakwa yake.”
Lokomotiv Moscow ni timu inayomilikiwa na shirika la reli nchini Urusi na ni moja ya timu ambazo zimewekewa vikwazo na nchi ya Marekani wiki iliyoisha, Markus Gisdol alichaguliwa kuwa kocha wa timu hiyo mwezi oktoba kipindi ambacho mkurugenzi wa michezo Ralf Rangnick alikuwa anahamia klabu ya Manchester United.
Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.