Marseille wametangaza visa tatu za Covid-19 baada ya kukamilisha vipimo ya waliokuwa wanahisiwa kuwa na Corona. Hii itaathiri moja kwa moja mipango ya kuanza kwa Ligue 1.

Wakiwa katika maandalizi ya kuelekea msimu mpya, Klabu hii ya Ligue 1 iliweka wazi Jumapili kuwa watu watatu ndani ya klabu wamegundulika kuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na COVID-19.

Wakati klabu ikitoa taarifa hii iliashiria wazi kuwa klabu ilikuwa inatafuta uthibitisho kuhusu visa hivyo na majibu ya vipimo yaliyorejea Jumatatu yote yalirudi yakiwa chanya.

Hii inafanya jumla ya visa za covid-19 za klabu ya Marseille kupanda hadi nne katika wiki iliyopita.

Marseille wapo katika maandalizi ya kuanza kampeni mpya 2020-21, walikuwa na mechi ambayo walitakiwa kuicheza Ijumaa dhidi ya Saint-Etienne. Kutokana na majibu haya, kuna uwezekano kuwa mechi yao wanayomkaribisha St. Etienne itachezwa Septemba 16 au 17.

Mechi ya Ijumaa ilipaswa kuwa mechi yao ya kwanza League 1 tangu Machi mwanzoni, wakati viongozi wa Ufaransa waliposimamisha michuano kwa sababu ya ugonjwa huo – mashindano hayo yalilazimika kumalizika rasmi Aprili 28.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi ucheze

35 MAONI

  1. Poleni sana kwa janga la corona linazidi kukandamiza nguvu ya vijana mungu awape nguvu wote mnaoumwa na ipo siku litatoweka kama kimbunga

  2. Duuuh! Kweny upande wa burudan ya michezo habari hii n ya kusikitisha sana kwan inatupa mtazamo tofaut uwenda wakasitisha tena burudan ya mpira

  3. Marseille wapo katika maandalizi ya kuanza kampeni mpya 2020-21, walikuwa na mechi ambayo walitakiwa kuicheza Ijumaa dhidi ya Saint-Etienne. Kutokana na majibu haya, kuna uwezekano kuwa mechi yao wanayomkaribisha St. Etienne itachezwa Septemba 16 au 17.

  4. Maisha yanatakiwa kuendelea hata baada ya kugundulika maambukizi mapya, hakuna sababu ya mechi kusimama kila inapobainika maambukizi mapya#merdianbettz

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa