Lisandro Martinez: Atoa Shukrani Man Utd.

Lisandro Martinez ametoa shukrani zake kwa wale wote waliohusika yeye kupata tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti 2022, ambaye amechukua tuzo hiyo na kuwa mchezaji wa kwanza wa Man Utd kuchukua tuzo hiyo kwa msimu huu 2022/2023.

Lisandro Martinez: Atoa Shukrani Man Utd.

Martinez aliposti shukrani zake kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo alisema kuwa

“Nawashukuru sana wale wote waliochangia mimi kupata tuzo hii, lakini upambanaji wa timu ni ufunguo wa mafanikio, tunapamba pamoja na tunachukua tuzo pamoja”

Lisandro Martinez: Atoa Shukrani Man Utd.

Lisandro amefanikiwa kuchukua tuzo hiyo akiwashinda wachezaji wenzake aliokua akichuana nao ambao ni beki Tyrell Malacia, pamoja na Raphael Varane,Hii imekuja baada ya kuonesha kiwango bora sana katika mechi za karibuni za klabu hiyo hasa mchezo dhidi ya Liverpool ambae alimaliza kama nyota wa mchezo.

Lisandro Martinez: Atoa Shukrani Man Utd.

Martinez alijiunga na Manchester United akitokea timu ya Ajax na kwa kipindi cha hivi karibuni amekuwa na kiwango bora sana kilichowavutia wengi sana.

Tuzo hii hutolewa kwa mchezaji aliefanya vizuri kwa mwezi huo na klabu hutoa nafasi mashabiki kuchagua kwa kupiga kura kupitia mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

Acha ujumbe