Aliyekua kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amemalizana na shirikisho la soka la Ureno ili kuanza kuifundisha timu hiyo kuchukua nafasi ya Fernando Santos.

Kocha huyo ambaye amekua akiifundisha timu ya taifa ya Ubelgiji ambayo ilikua na kizazi bora kabisa wengi wakikiita kizazi cha dhahabu. Martinez amekua kocha wa Ubelgi kwa muda mpaka kufikia kuachana na timu hiyo baada ya kutupwa nje kwenye michuano ya kombe la dunia.martinezKocha huyo raia wa kimataifa wa Hispania ambaye amewahi kuvifundisha vilabu vya Wigan, Everton vyote kutoka nchini Uingereza katika utumishi wake ndani ya timu ya taifa ya Ubelgiji mafanikio aliyoyapata ni kushinda nafasi ya tatu kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Timu ya taifa ya Ureno ambayo kwa sasa haina kocha mkuu baada ya aliyekua kocha wake Fernando Santos kuachana na timu hiyo baada ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la dunia hatua ya robo fainali, Na kocha Roberto Martinez anatajwa kuchukua nafasi ya kocha ya Fernando Santos.martinezMakocha kadhaa wametajwa kuchukua nafasi ya kuchukua kibarua cha kuifundisha timu ya taifa ya Ureno ikiwemo kocha Mreno Jose Mourinho, Lakini taarifa kutoka nchini Ureno zinaeleza Kocha Martinez ameshakubaliana na shirikisho nchini humo kuchukua kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Ureno.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa