Mashabiki 10 wa Liverpool Wakamatwa na Polisi

Idadi kubwa ya mashabiki wa Liverpool walijitokeza kushangilia ushindi wa taji la Ligi Kuu baada ya kusubiri kwa miaka 30.

Polisi walilazimika kuwatia nguvuni mashabiki 10.

Licha ya kuendelea kuwepo kwa masharti ya kutokukusanyika, mashabiki wa Liverpool uzalendo uliwashinda wakishindwa kuzuia hisia zao.

Mashabiki 10 wa Liverpool Wakamatwa na Polisi
Mashabiki walijitokeza kwa wingi wakiimba nyimbo za kuisifu Liverpool na wakipiga baruti katika shamra shamra za shangwe la ushindi

Mashabiki hawa wamesubiri kwa mda mrefu timu yao kuinua taji la EPL. Na mara baada ya kutangazwa washindi, huku wakiwa wamebakiza mechi 7 mkononi, mashabiki waliingia mtaani.

Askari wa Merryside waliwatia nguvuni watu mashabiki 10 kwa makosa ya kukiuka maagizo kwa umma, usiku ambao shangwe za kuondokana na ukame wa mataji Liverpool zilitawala.

Mashabiki 10 wa Liverpool Wakamatwa na Polisi
Mashabiki hawakuzingatia sharti la kukaa umbali wa mita 1.

Maelfu ya mashabiki walijitokeza pale Anfield na katikati ya jiji baada ya kutangazwa ubingwa. Baada ya Chelsea kuwatandika Man City bao 2-1, mashabiki walianza kufurika nje ya uwanja. Idadi ilizidi kuongezeka huku mashabiki wakipuuza sheria ya kukaa umbali wa angalau mita 1.

 

 

 

44 Komentara

    Wanastahili ni miaka mingi Sana katika soka hawajaligusa wala kulisikia saivi ni wakati wao

    Jibu

    Da wamesota kwa miaka mingi sana hivyo wanahaki yakushangilia

    Jibu

    Hii n furaha kubwa sana kwa mashabiki wa Liverpool kwa waswahil tunasema adui wako muombee njaa atakuheshim tu ata Kama alikuwa shujaa ndo kitu kilichowakuta club ya man city walivyokuwa wakicheza dhid ya Chelsea n mchezo ambao kila mtu alikuwa anahamaki kuangalia man city watafanye waweze kutwaa point hzo ila matokeo dak 90 ndipo Chelsea alivyofanya maajabu kuitandika man city na kuifanya kupoteza point muhim
    Mashabiki wa Liverpool wako nafuraha kubwa sana ya kutangaza ubingwa takriban miaka 30 hivy walikuwa wanaisikia EPL
    Nice update 👍
    # meridianbet Tanzania

    Jibu

    Uzalendo umewashinda mashbk wa liverpool

    Jibu

    Duhh Hawa mashabiki wa Liverpool kweli no Nina kocha ya kiwepo na corona bado wanaeshangilia tu mitaana

    Jibu

    Muda sana hawajalishika saivi niwakati wao

    Jibu

    Hii makala mzuri sn

    Jibu

    dah hawa jamaa yaani walikuwa na kiu sana na ubingwa wamechukua kipindi kizur cha corona maana wangefanya sana fujo

    Jibu

    Muda Sana hawajalishika kwa Sasa ndio muda wao

    Jibu

    Wawaachilie tu hao mashabiki walionyesha hisia zao jamani,ni mda mrefu sana ulipita kwa Liverpool na sasa ni mabingwa

    Jibu

    Duu. Mashabiki wa Liverpool siku zote wanapenda vurugu .waache wakamatwe.

    Jibu

    Walistahili ubingwa kwa club ya Liverpool kwa takriban miaka 30 bila kua na kombe la ligi kuu uingereza na mashabiki walikua na hamu kubwa kuona jambo likitokea kwenye club yao mpira ni hisia na hisia humfanya mtu akafanya vitu ambavyo hata mwenyewe hakukusudia ilq tahadhali muhimu hasa kipindi hiki cha covid 19

    Jibu

    Mengi yatajitokeza kwa wadau wa klabu ya liver kutua ubingwa asa England

    Jibu

    Mashabiki wa riverpool uzalendo uliwashinda wameshindwa kuzizuia hisia zao

    Jibu

    Walivumilia vya kutosha waacheni wafurahie

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Mashabiki was Liverpool wanafuraha kubwa sana ya kutangaza ubingwa walio kua wanausubir takribani miaka 30 walikua wanaisikia sikia tu EPL

    Jibu

    Askari wamefanya makosa wasingewakamata sababu ni wanashangilia ushindi wao waliouoambania kwa muda mrefu

    Jibu

    Viva Liverpool#meridianbettz

    Jibu

    Ni habari mbaya Sana hizi tatizo wa shabiki wa Liverpool wanavulugu sana

    Jibu

    Jmn raha zimewazidi.wawaache tu

    Jibu

    Haaah jamani hawajatendewa haki kwan walimic sana gem na ndio maana wakashindwa kujizuiya wakajikuta wanashangilia#meridianbettz

    Jibu

    Duu mashabiki waliverpool wanapenda ushangiliaji wavulugu ndomana Wana kamatwa

    Jibu

    duuh hatar watu wameshangweka adi wanakatwa

    Jibu

    uzalendo umewashinda wameahindwa kuzuia hisia zao

    Jibu

    Mda mrefu wawaache tu washangilie maana wameliangaikia htr

    Jibu

    Mashabiki wa Liverpool wanajulikana duniani kwa mzuka. Ni jambo la kufurahisha kupata kombe baada ya kusubiri miaka 30#meridianbettz

    Jibu

    Yani wasingeweza kuzuia hisia zao mashabiki wa Liverpool wanajulika

    Jibu

    Hii issue ya social distance kwa nchi za wenzutu imekuwa changamoto sana, Lakini kwa mashabiki wa Liverpool walikuwa na haki ya kushangilia hivi maana ni furaha iliyopitiliza kwao, Miaka 30 sio mchezo!!!!

    Jibu

    Wawaachie tu watu wako na furaha jamani

    Jibu

    walikua na hamu kubwa kuona jambo likitokea kwenye club yao mpira ni hisia na hisia humfanya mtu akafanya vitu ambavyo hata mwenyewe hakukusudia ilq tahadhali muhimu hasa kipindi hiki cha covid 19

    Jibu

    Miaka 30 ming acha wafurah tu

    Jibu

    Waachwe huru tu coz ni katika kushangilia

    Jibu

    Waache wafurah 30 wamelipata leo duh

    Jibu

    Acha tu jamani walikuwa na Ukame sana #Meridianbettz

    Jibu

    Nguvu ya shabiki hahahaha uongozi utafanya utaratibu watawalipia fine watatoka

    Jibu

    Wasamehewe tu,mana sio kosa lao furaha imezidi kina.

    Jibu

    Duuu kwahiyo ndouzalendo uliwashinda ?

    Jibu

    Kwakwer fulaha yao aiwez vumilika

    Jibu

    Ni furaha kubwa sana kwa mashabiki walishindwa kuzuia hisia zao mpaka wamejisahau kama kuna sheria ambazo zimeweka wasamehewe tu mana hawakukusudia kufanya kosa ila uzalendo uliwashinda kuvumilia hizia zao kwa miaka mingi walisubitia kwa hamu kubwa hivyo sasa wameokota dodo

    Jibu

    Ila kwa ukamu wa kombe hapa mashabiki tena hawaangalii korona maana miaka 30 Dah sio poa furaha mpaka imezidi kina na kwakuwa korana imewaaribia sana wangejirusha sana kombe limekuja mda mbaya kwao ila sio kesi wamefurahi na polisi wawaachie tu hao mashabiki muamko ndio imefanya wasiwezee kukaa mita moja

    Jibu

    Muda sana nifuraha ilioje

    Jibu

    Waache wafurahi maan wamevumulia kwa kipindi kirefu San nifurah iliyopita kifan

    Jibu

    Furaha ikizidi mwisho majonzi

    Jibu

Acha ujumbe