Kuelekea debi kali kabisa Italia kati ya Lazio na mahasimu wao Roma, mashabiki wa Lazio wametangaza mgomo kushinikiza klabu kuchukulia uzito suala la kuuwawa kwa shabiki wao.
Taarifa zilizobamba katika jiji la Roma mwezi uliopita zinadai Fabrizio Piscitelli ambaye ni maarufu kama Diabolik, aliuwawa kwa kupigwa risasi ya kichwa. Askari wa jiji hilo walidai kisa hiki kuwa ulikuwa ni mpango wa kumuua bwana huyu. Bwana huyu alikuwa shabiki maarufu wa Lazio.
Kutokana na kufahamika kwake kama shabiki wa Lazio na baadhi ya makundi yanashinikiza uongozi watoe heshima kwa kuupa uzito msiba wake.
Diabolik alikuwa anahusishwa na magenge kadhaa ya kihalifu, inadaiwa huenda hao ndiyo waliopanga kumuangamiza. Pia, baadhi ya makundi yamenukuliwa ayakisema bwana huyu alikuwa tayari ameshaondoka kwenye mtandao wa uhalifu kwa mda mrefu.
Mashabiki wanahitaji klabu ya Lazio itoe tamko rasmi kwa umma kuhusu kulaani suala hilo na hata kutoa mda wa ukimya kabla ya mechi kwa ajili ya kumkumbuka shabiki wao. mashabiki wamedai kuwa hawatashangilia hata kama wakipata goli au wakipata ushindi kabla au baada ya mechi.
Furahav
Majanga