Hili Sharti Neymar Kurejea Barca Limemshinda?

Dondoo za masuala ya usajili zimekuwa zikimuhusisha Neymar na kusepa PSG akionekana ameshachoshwa na mshike mshike wa Ligue 1. Neymar alikuwa anahusishwa sana na klabu ya Real Madrid na klabu yake ya zamani ya Barcelona. Taarifa zinadai kuwa Neymar amepewa masharti kadhaa ikiwa anataka kurejea Barca.

Taarifa zinadai kuwa staa huyu alichagua kurejea Barcelona kuliko kwenda Real Madrid. Neymar akiwa PSG, katika msimu uliopita alikukutana na kipindi kigumu sana, pengine ni kigumu zaidi katika soka lake la kulipwa baada ya kupata mikiki mikiki ya majeraha na kujikuta akitumia mda mrefu nje ya uwanja.

Klabu ya Barca, waliripotiwa kuwa wapo tayari kumpokea kijana wao ambaye pia amekiri kuwa kuondoka klabuni hapo ilikuwa ni kosa. Lakini ili aweze kurejea kuivaa jezi ya Barcelona, moja ya masharti ambayo ni lazima akubaliane nayo ni kupungua kwa mshahara.

Soko la uhamisho wa wachezaji linatarajiwa kupigwa vibaya na janga lililoikumba ulimwengu ambalo kwa nafasi yake limeleta athari kubwa katika ulimwengu wa soka na uchumi wa vilabu.

PSG wanajiandaa kumbakiza Neymar na mwenzake Kylian Mbappe na wapo tayari kujitahidi kuwapa kile watakachohitaji. Ikiwa mastaa hawa wataondoka kwa namna yeyote PSG, lazima watakuwa wamepata ofa nzuri zaidi, je ni klabu gani kwa hali ya sasa ipo tayari kuwalipa mishahara mikubwa wanayolipwa PSG ukiacha ada zao za uhamisho?

Kiuhalisia klabu ya Barcelona haifanani na klabu ya PSG kiuchumi, PSG wakitajwa kuwa na pesa zaidi, hivyo Barcelona hawataweza kumlipa Neymar malipo yale yale aliyokuwa akilipwa na PSG.  Hivyo kupunguzwa mshahara ni kipaumbele ili staa huyu aivae jezi ya La Liga tena! Ungekuwa yeye?

Barcelona wanamuhitaji nyota huyu pia kukubali kutolipwa baadhi ya bonasi. Wadau wanaamini huenda staa huyu akarejea relini kama akirejea Barcelona kwa sababu ya uwepo wa Messi Barcelona, wawili hawa wanaiva sana wakiwa pamoja.

46 Komentara

    Kila mtu anaangalia maslai yake ye km anaona hamlipi ana sababu yakukataa

    Jibu

    Harud nyumban tumemic sana vitu vyake Asante meridian kwa habar ya kimichezo

    Jibu

    Psg ndo pakukomaa akaze tu

    Jibu

    Kila mtu anaangalia maslai yake

    Jibu

    Muda wake unaisha sasa

    Jibu

    safi. fundi wa mpira brazil & psg# meridianbettz

    Jibu

    Bora abaki psg kama Barça wanazingua

    Jibu

    Apambane tu PSG

    Jibu

    Abakie tu p,s,g ndo panamfaa

    Jibu

    Bora asikilize moyo wake kama unataka arudi Barcelona basi arudi tu

    Jibu

    Psg aneangalia masilai

    Jibu

    arudi tuu nyumbani tumemmic sana

    Jibu

    abaki psg

    Jibu

    Huyo bishooo abaki PSG tu

    Jibu

    Ridhki popote abaki tu PSG

    Jibu

    PSG nayo ni timu kubwa atulie tu #meridianbettz

    Jibu

    arudi tu barca

    Jibu

    Arudi Barcelona

    Jibu

    Bora aende epl kuliko kwenda laliga epl Kuna timu kibao zinamuitaji pia atokutana na hayo makato yote na atakuwa mchezaji wakuangaliwa muda wote

    Jibu

    Muamuzi ni yeye Kama masilai yanalipa arudi barca

    Jibu

    Bora aende epl kuliko kwenda laliga epl Kuna timu kibao zinamuitaji pia atokutana na hayo makato yote na atakuwa mchezaji wakuangaliwa muda wote#meridianbettz

    Jibu

    Aende tu.

    Jibu

    Inavyoonekana Barcelona hawamuhitaji kama wangemuhitaji wangekubaliana mshahara kwa sababu ya kiuchumi lakini kuweka mashariti sio sahii

    Jibu

    Huyu mpenda pesa hawezi kukubali kupunguza mshahara wake

    Jibu

    Huyu mpenda pesa hawezi kukubali kupunguza mshahara wake huyu bishoo

    Jibu

    Arudi tu nyumbani maana tumemiss Sana 3 twin warudi Kama zamani

    Jibu

    Kwa kiwango chake kwa Sasa ni Bora tu angekubali kupunguziwa mshahara Barca akifanya vizuri na Barca Bado wakiwa wanamuhitaji ataongezewa tu.

    Jibu

    Arud Barca nafas yake bado ipo

    Jibu

    Arudi tu nyumbani tume miss sana

    Jibu

    Neymar bishoo sana..!ubishoo ukizidi sana utaaribu kipaji chako acha ustaa

    Jibu

    Arudi tuu Barca

    Jibu

    Hapa Neymar anawakati mgumu sana, anakazi ya kuchagua swala la mapenzi na klabu na Mkwanja!!!!

    Jibu

    Arudi nyumban

    Jibu

    kuangalia maslai ni vizuri lakini Mimi namshauri abaki tu psg

    Jibu

    Kwake limekuwa Shakti kubwa Ndio maana limemshinda

    Jibu

    Nimekuwa nikishuhudia maamuzi mengi mabaya ya wachezaji wa Brazil wakati wa usajiri. kama Neymar hajapata alilotaka akiwa PSG sioni maajabu atakayopeleka Barcelona.

    Jibu

    Masharti yao magumu ,ila kama mwenyewe karidhia basi sio mbaya.

    Jibu

    Kwaajili ya ulinzi wa kipaji chake akubali tu hayo masharti

    Jibu

    Messi anakubalika sana barcelona na kipaji chake kitakua sana kuliko psg

    Jibu

    Ni bora arudi barca

    Jibu

    Messi anakubalika sana Barca

    Jibu

    Hana jipya abaki PSG

    Jibu

    Harud nyumban tu Asante meridian

    Jibu

    Rudi nyumbani messi

    Jibu

    Arudi alipotoka bhna

    Jibu

    Bora arudia maana tumemic mambo yake
    #meridianbet

    Jibu

Acha ujumbe