Franco Mastantuono amesema kuwa ni “heshima kubwa” kwake kuweka historia akiwa Fiorentina, baada ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga hat-trick katika mchezo wa mashindano akiwa na klabu hiyo ya Tuscany.
Mchezaji huyo wa Real Madrid aliye kwa mkopo alifunga mabao matatu katika ushindi wa Fiorentina wa 4-2 ugenini dhidi ya Venezia Ijumaa usiku.
Matokeo hayo hayakuwa tu ushindi wa kwanza wa Fiorentina msimu huu na ushindi katika mchezo wa kwanza wa Paolo Vanoli tangu arejee kwa mara ya ‘pili’ kama kocha wa timu hiyo, bali pia yalimfanya Mastantuono, mwenye umri wa miaka 19, kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga hat-trick akiwa amevalia jezi ya Viola.
“Kwangu mimi, ni heshima kubwa kuingia katika historia ya klabu kubwa na yenye hadhi kama hii,” Mastantuono aliiambia DAZN kupitia LaViola. Leo ilikuwa muhimu kupata matokeo, na tulicheza mchezo mzuri sana. Ninafurahia ushindi, mbali na suala la mabao.”
Haishangazi kwamba Mastantuono alipewa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi na Serie A, lakini mchezaji huyo wa Real Madrid aliye kwa mkopo aliamini kuwa Nicolò Fagioli pia alistahili tuzo hiyo.
“Alifanya vizuri sana, kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengine wote wa timu. Ninafuraha sana na ushindi huu”. A lisema Mwaargentina huyo.
Mastantuono alijiunga na Fiorentina kwa mkopo wa moja kwa moja kutoka Real Madrid mwezi Agosti. Hii inamaanisha kuwa Fiorentina haina kipengele cha kumnunua moja kwa moja na kumfanya uhamisho wake kuwa wa kudumu mwishoni mwa msimu.
Mastantuono alijiunga na Real Madrid akitokea River Plate kwa ada ya uhamisho ya euro milioni 45 mwaka mmoja tu uliopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 tayari amefikisha idadi sawa ya mabao aliyofunga akiwa Real Madrid msimu uliopita, ambapo alifunga mabao matatu katika mechi 35 alizoicheza kwenye mashindano yote, huku akitoa pia asisti moja.