Timu ya Galatasaray imekamilisha usajili wa Juan Mata kama mchezaji huru akitokea Manchester United. Juan Mata atasaini mkataba wa mwaka mmoja katika timu hiyo. Na mchezaji huyo anacheza nafasi ya kiungo katika timu yake hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha mpya Ten Hag.

 

Mata(34) Kujiunga Galatasaray

Juan Mata amecheza muda mrefu ligi kuu ya Uingereza ambapo alicheza katika klabu ya Chelsea pia kabla ya kujiunga na mashetani hao wekundu. Mata imekuwa ni ngumu kwake kupata nafasi katika timu hiyo ya United kutokana na kutokuwa chaguo la kwanza la kocha, lakini vilevile kuwepo kwa wachezaji wenye uwezo kuliko yeye.

Mchezaji huyo  anaenda Galatasaray baada ya kumalizana na Old Traford na kuonekana kuwa timu hiyo haina mpango wa kuendelea nae, pia umri wake wa miaka 34 hauruhusu yeye kuendelea kuitumikia klabu hiyo kutokana na falsafa ya mwalimu kutaka vijana wenye umri mdogo ili kuijenga timu hiyo.

Mata, Mata(34) Kujiunga Galatasaray, Meridianbet

Galatasaray ambayo inashiriki ligi ya Uturuki ijulikanayo kama (Super Lig ) imeshacheza michezo mitano, imeshinda mitatu, sare moja, na kupoteza mchezo mmoja. Na katika msimamo wa ligi ipo nafasi ya 7.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa