Klabu ya Simba SC leo inashuka katika Uwanja wa Orlando nchini Afrika Kusini kuikabili Orlando Pirates katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa majira ya saa moja jioni.
Pablo amesema Wanasimba na Watanzania kwa ujumla wanatamani kutuona wakivuka nusu fainali kitu ambacho wamejipanga kukitimiza leo.
“Imepita miaka 29 tangu tulipocheza fainali ya michuano hii. Watanzania wanatamani kuiona timu yao ikifika hatua hii na tumejipanga kuhakikisha tunapita kwa kuitoa Orlando,” amesema Pablo.
Orlando Pirates ndio timu pekee ya Afrika Kusini iliyosalia katika mashindano ya CAF baada ya hapo jana Mamelodi Sundowns kutolewa na Petro de Luanda kwa wastani wa magoli 2-3.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.