Klabu ya Simba SC leo inashuka dimbani kuvaanana klabu ya Orlando Pirates katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaopigwa majira ya saa moja usiku katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kocha wa Simba SC, Pablo Franco, amesema kikosi kiko tayari kwaajili ya mchezo huo na anaamini hali ya uwanja itakuwa faida kwetu kutokana na ruhusa kutoka Shirikisho la Soka Afrika CAF la kujaza uwanja.

 

simba sc, Matchday : Simba SC vs Orlando Pirates., Meridianbet

Pablo amesema anajua shauku ya Watanzania na mashabiki wa Simba SC kutaka kuona timu ikitinga nusu fainali baada ya kupita miaka zaidi ya 20.

“Tunacheza kwa kutafuta nafasi ya kufuzu nusu fainali siyo pointi, kwa hiyo tutahakikisha tunatumia vizuri nafasi tutakazopata ili kumaliza mchezo katika uwanja wa nyumbani.

 

“Kuhusu kikosi kipo tayari, tumefanya mazoezi na wachezaji wapo katika hali nzuri. Tunajua Wanatanzania wanahitaji kuiona timu ikiingia nusu fainali baada ya kupita muda mrefu nasi tutahakikisha tunafanikisha hilo.

 

“Hii ni mechi ya mtoano hatuhitaji pointi. Tunahitaji mtaji mkubwa wa mabao nyumbani hivyo tunapaswa kutumia nafasi tutakazopata ili kujiweka kwenye nafasi nzuri mechi ya marudiano,” amesema Pablo.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa