Beki wa zamani wa Inter, Marco Materazzi ameishukuru Milan kwa kumruhusu Hakan Calhanoglu kuondoka na kujiunga na wapinzani wao wakuu ndani ya Serie A.

 

Materazzi: "Asante Milan kwa Kumuachia Calhanoglu Kwenda Inter"

Kiungo huyo wa kati wa Uturuki mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Nerazzurri mwaka jana baada ya kuondoka Rossoneri kwa uhamisho huru, akiwa ameitumikia Milan kwa miaka minne akiwa amevalia uzi wa Milan.

Mchezaji huyo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Simone Inzaghi, akifunga mabao 10 na kutoa asisti 16 katika mechi 61 jumla za klabu.  Akizungumza na InterTV kabla ya mechi ya Nerazzurri dhidi ya Viktoria Plzen, Materazzi alitoa mawazo yake kuhusu Calhanoglu na kuondoka kwake Milan mwaka jana. Materazzi amesema;

“Lazima tuwashukuru wapinzani wetu ambao walimwacha kwa ajili yetu na ambao wanaongea sana. Hatuna budi kumshukuru, ni mtu ambaye huongea kidogo lakini anafanya vitendo”.

Materazzi: "Asante Milan kwa Kumuachia Calhanoglu Kwenda Inter"

Calhanoglu mwenye umri wa miaka 28 amecheza michezo 15 katika Serie A na Ligi ya Mabingwa msimu huu, akifunga mabao mawili na kutoa asisti tatu kwa wakati huo. Amekuwa mtu muhimu kwenye safu ya kiungo, akiruhusu wachezaji wenzake kama Nicolo Barella na Lautaro Martinez kung’aa.

Inter sasa wamejikatia tiketi ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wao dhidi ya Viktoria Plzen, huku Milan wakiwa bado wanahitaji kupata matokeo chanya dhidi ya RB Salzburg wiki ijayo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa