Matukio ya Kushangaza Yaliyowahi Kutokea Kombe la Dunia

Kuna mambo hutokea kwenye mechi kubwa kama hizi za kombe la dunia na kuibua taharuki kwa baadhi ya mashabiki na viongozi mbalimbali wa soka. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yaliwahi kufurahisha na kushangaza dunia kwa namna yalivyoweza kutokea kwa kipindi fulani hasa ikizingatiwa ni katika michuano hiyo mikubwa.

Clive ‘The Book’ Thomas ni refa aliyechezesha mechi kati ya Brazil na Sweden mwaka 1978 na kufanya tukio ambalo lilifurahisha ulimwengu mzima; katika mechi ile matokeo yalikuwa ni 1-1 na wakati mechi inaelekea kumalizika ulipatikana mpira wa adhabu ambao ulikuwa eneo la karibu sana na maeneo ambayo sio rahisi kwa mchezaji kukosa kufunga. Kwa wakati huo akapuliza kipyenga chake kuashiria ilikuwa ni faulo, ikaruhusiwa kupigwa lakini wakati goli linafungwa na mchezaji hatari wa kikosi hicho cha Brazil, Zico refa huyo alimaliza mechi ile na kukataa kabisa goli lililofungwa kwamba: halikuwa ndani ya muda wake. Na kufanya mechi ile kumalizika kwa sare ileile.

Maradona kuonekana anatumia madawa, katika fainali zile za 1994 mchezaji huyo alikuja kugundulika anatumia madawa yanayopigwa vita uwanjani na kwa wachezaji kitu ambacho kiliweza kumfanya arudishwe nyumbani kwa aibu baada tu ya kucheza mechi kati yao na Ugiriki, ambapo hakuwa mbali na aliweza kudhihirisha ubora wake kwa kuwafunga miamba hao. Lakini pia aliweza kufungiwa miezi 15 kwa tukio lile lakini pia, baada ya adhabu hiyo alipokuja kupimwa tena kabla ya mechi na Nigeria aliweza kudhihirika kwa mara nyingine tena kuwa bado anatumia madawa hayo.

Ronaldo kuachwa nje ya kikosi 1998, pamoja na ubora wake ambao una historia ndefu duniani kutokana na ufundi wake mkubwa uliotukuka, mchezaji huyo aliweza kuachwa katika kikosi kilichopangwa siku ya fainali kati yao na Ufaransa, jambo ambalo lilionekana kuwashtua mashabiki wengi wa Brazil kutokana na uwezo wa mchezaji huyo na historia yake. Ilikuja kudhihirika kwamba hakuwepo kabisa kwenye karatasi za utambuzi wa kikosi kinachocheza kwa siku husika, japo waliibuka washindi pale. Lakini baadae ilikuja kutambulika kwamba alikuwa amepata majeraha yliyolazimisha yeye kukaa nje.

Salaam ya ki-fasisti ya timu ya taifa ya Italia, ilikuwa ni katika mechi ya fainali kati ya Italy na Ufaransa mwaka 1934 ambapo Italia walikuwa wenyeji wa mechi ile na kufajijiwa kuibuka na ushindi mnono kwenye mechi yao. Kabla na baada ya ushindi huo waliweza kufanya matendo yote yaliyokuwa ya kisiasa zaidi kwa sababu kwa kipindi hicho kulikuwa bado na chembe za utawala wa Kifasisti chini ya Benito Musollini, na hata sare zao zote zilikuwa zimewekewa alama ya chama hicho. Baada ya tukio hilo miaka minne baadae waliweza kusogea kwa mara nyingine na kukutana tena na Ufaransa kwenye fainali kutetea kombe hilo lakini walishindwa kufanya hivyo na kupoteza mechi yao mbele ya wafaransa.

Hayo ni baadhi ya mengine mengi yaliyovunja rekodi katika michuano hiyo mikubwa duniani, kuwahi kutokea kwenye soka.

2 Komentara

    Gud news

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

Acha ujumbe