Matunda ya Klopp

Kazi kubwa ya makocha ni kuwafanya wachezaji kuwa na nafadi kubwa ya kufanya vizuri na kuonesha ile siri yao ya ndani kiuwezo katika kuisaidia timu. Klopp ni kati ya makocha ambao wameweza kufanya makubwa sana katika historia ya soka kwa kugeuza wachezaji wenye uwezo wa kati kuwa nyota bora zaidi wanaoheshimika.

Baadhi ya wachezaji waliopita kwenye mikono ya kocha huyo hawakuwa na majina makubwa ambayo yangekuwa na upekee wowote lakini wamekuja kuleta mabadiliko makubwa kisoka na kuanza kuwindwa na kufanya vizuri zaidi mwenye klabu walimo. Wafuatao ni baadhi ya wachezaji waliokuwa chini ya utawala wa kocha huyo na wakawika sana.

Robert Lewandowski, jina la nyota huyo linakumbukwa sana kipindi alipokuwa chini ya utawala wa Klopp pale Dortmund. Ni aina ya wachezaji ambao walikuwa na vinasaba vya kujua goli lilipo na historia hiyo badl anaendelea nayo. Kabla ya kuhamia Bayern aliwafungia Dortmund magoli 103 kwenye mechi 187 chini ya Klopp.

Mats Hummels, pamoja na kwamba lilikuwa ni zao la Bayern lakini alijiunga kwa mkopo na klabu ya Dortmund na kufanikiwa kujenga heshima kubwa sana ndani ya klabu hiyo. Baada ya kujiunga kwa mkataba na Dortmund mwaka 2009 chini ya Klopp aligeuka kuwa kisiki katika safu ya ulinzi na kungara sana kabla hajarudi Bayern.

Marco Reus, mbali na majeraha ambayo nyota huyo amekuwa akikutana nayo mara kwa mara: lakini akiwa kwenye utimamu wake amekuwa gumzo sana ndani ya klabu hiyo. Uimara wa nyota huyo ulianza tangu kipindi cha Klopp alipokuwa ameshikilia mikoba ya klabu hiyo. Heshima yake bado ipo kwa nyoya hao ambao aliwaamini na wakafanya vizuri sana.

Mario Gotze, pamoja na kwamba bado wamesalia kuendeleza gurudumu la Borissia lakini kazi kubwa sana iliweza kufanywa na Klopp kutengeneza majina hayo hadi hapo walipo kwa sasa. Wanaweza kuaminiwa kutokana na uwezo wao ambao kwa hakika kocha huyo aliweza kuwajengea na kuwatemgeneza kuwa bora zaidi.

Mbali na nyota hao kuna wachezaji wengine chini ya gurudumu hilo wakiwemo; Philippe Coutinho (Liverpool), Sadio Mane (Liverpool), Shinji Kagawa (Dortmund), Nuri Sahin (Dortmund), Roberto Firmino (Liverpool) na  Ilkay Gundogan (Dortmumd) lakini thamani yake ikaweza kuonekana nje ya mipaka ya klabu hiyo, na anahudumu chini ya Pep kwa sasa kwa kiwango cha pekee sana.

2 Komentara

    Hongera kwa klopp

    Jibu

    Kloop yupo vzr sana

    Jibu

Acha ujumbe