Hakika kizuri chajiuza. Licha ya kuwa anacheza Championship, beki wa klabu ya Norwich City – Max Aarons anawachachafya wakurugenzi wa michezo kwenye vilabu vikubwa barani ulaya.
Aarons (miaka 21) anatajwa kama mchezaji mwenye nyota njema akiwa kama beki hodari wa pembeni. Vilabu kadhaa ikiwemo Man United, Barcelona, Bayern Munich na AS Roma vimehusishwa na Aarons katika vipindi tofauti tofauti.
Imeripotiwa kuwa, Everton nao wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka Aarons ambaye wanamtizama kama mrithi sahihi wa nahodha wao – Seamus Coleman. Ifikapo mwezi Julai, 2021 Coleman atakuwa amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake na Everton.
Licha ya kuwa Norwich City haichezi Ligi Kuu nchini Uingereza, klabu hiyo haitopokea dau lolote la chini ya pauni milioni 30-35 kama sehemu ya usajili wa Max Aarons.
Nani ataibuka kidedea kwenye mchakato wa usajili wa Aarons katika siku za usoni?
TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET
BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.
Duuh
Sasa itakuwaje
Sijui itakuwaje
Hiyo balaa
Asante kwa taarifa
Mmh kazi ipo
Mwenye mkwanja atampata
Katisha