Gwiji wa Soka la Tanzania, Ally Mayay Tembele amefunguka kuwa taarifa za kuteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Tanzania zilikuja kwa kushtukizwa na hakuwa na tetesi za kuwa atapewa nafasi hiyo.
Mayay Afunguka Kushtukizwa Kuwa Bosi BMT

Mayay alisema: “Kiukweli sina taarifa, wewe ndiye unanipa ‘breaking news’ hii sina taarifa kabisa na ninakosa hata jambo la kuongea na kuzipokea pongezi hizo ambazo unanipa. Imenishitua sana habari hii unayonipa.

“Sikuwa na tetesi na sikuwa kugusiwa kuwa nafikiriwa kupewa nafasi hiyo kubwa ya uongozi wa masuala ya michezo nchini. Lakini naweza kusema asante kwa nafasi hiyo kama kweli kwa sababu ni jambo kubwa kwangu hata kama nimeteuliwa kwa kushtukiza.”

Mayay aliteuliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo akichukua nafasi ya Yusuph Omary Singo aliyepangiwa majukumu mengine.

Mayay Afunguka Kushtukizwa Kuwa Bosi BMT
Kabla ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo Mayay alikuwa Afisa Mwandamizi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania huku akifanya kazi ya uchambuzi wa soka katika kituo cha Azam TV na vituo vingi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa