Mbappe: Hatma Yangu Itafahamika Kabla ya Euro

Mshambuliaji wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe ameweka wazi kua hatma yake itafahamika mapema kabla hata michuano ya Euro kuanza mwezi June mwaka huu.

Mbappe anasema kabla ya michuano ya Euro atakua ameshaweka wazi ni wapi ataelekea msimu ujao, Kwani mpaka sasa inafahamika mchezaji huyo hatakua sehemu ya kikosi cha PSG msimu ujao kwani ameshatangaza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.mbappeKinachosubiriwa kwa hamu ni kujua ni wapi utakua uelekeo wa mshambuliaji huyo matata kabisa wa timu ya taifa ya Ufaransa, Yeye mwenyewe akisema klabuni kwake suala la yeye kuondoka sio mada tena kwani alishatanabaisha ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Staa huyo anasema lengo la kuweka wazi mustakbali wake kabla ya michuano ya Euro itakayofanyika mwezi Juni mwaka huu kule nchini Ujerumani ni kua sawa kiakili, Kwani anahitaji aweke kila kitu sawa ili awe sawa kiakili na kufanya mambo makubwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano hiyo.mbappeMpaka sasa taarifa zinaeleza Mbappe ameshakubaliana na klabu ya Real Madrid mpaka kiwango cha mshahara, Huku suala lililobakia ni kutangaza tu yeye mwenyewe ataelekea wapi msimu ujao lakini asilimia kubwa mchezaji huyo atajiunga na miamba hiyo ya soka kutoka nchini Hispania ambayo imekua ikimfukuzia kwa muda mrefu sasa.

Acha ujumbe