Mbappe: Nataka Kutengeneza Historia Yangu

Nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa na mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Kylian Mbappe amesema kua hafikirii kua mrithi wa Cristiano Ronaldo ndani ya Real Madrid badala yake anataka kutengeneza historia yake.

Mbappe akifanya mazungumnzo leo kuelekea mchezo wa robo fainali ya michuano ya Euro 2024 ambapo watacheza na timu ya taifa ya Ureno na atakutana na Ronaldo ambaye amekua akimtazama kama kioo kwake, Staa huyo ameweka wazi anamkubali sana Ronaldo lakini hafikirii kua mrithi wa mchezaji huyo gwiji ndani ya Real Madrid.mbappe“Nina fursa ya kuanza ndoto yangu ya kuchezea Real Madrid, natumaini kuandika historia ya Real Madrid.”

“Lakini hadithi ya Cristiano katika Real Madrid ilikuwa ya kipekee. Natumaini kufanya kitu cha kipekee. Nina sifa tu kwake. Tuko mawasiliano, yeye ni nguli.”

Watu wengi wanamuona Mbappe kama mrithi wa Cristiano Ronaldo ndani ya klabu ya Real Madrid na wakiamini alitakiwa kujiunga mapema zaidi na timu hiyo, Lakini mchezaji huyo kwa upande wake anaamini anapaswa kwenda kutengeneza historia yake mwenyewe ndani ya klabu ya Real Madrid.

Acha ujumbe