Mshambuliaji wa kutegemewa wa Liverpool, Mohamed Salah, asemwa kuwa na athari hasi kwa wachezaji wenzake kutokana na mbio zake za kutaka kuchukua kiatu cha dhahabu kwa ufungaji bora wa msimu.

Uchezaji wa timu ya Liverpool umekuwa ukizuazua kwa muda sasa huku wakiwa nafasi ya sita ikiwa na alama 57 nyuma ya West Ham wenye alama 58 wakiwa mbele kwa mchezo mmoja.

mbio za Salah Aweka Rekodi Mpya ya Mabao Liverpool

Uhakika wa Liverpool kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao ni moja ya miujiza mikubwa inayosubiriwa kwa hamu kubwa. Mchambuzi wa BBC, Garth Crooks anaamini kwamba Liverpool inaathiriwa kwa kiwango kikubwa na mchezaji mmoja mmoja, akiwemo kiongozi wa magoli wa klabu hiyo Mohammed Salah.

Salah anashika nafasi ya pili kwa wafungaji bora wa EPL akiwa na magoli 20 nyuma ya kinara Harry Kane ambaye ana magoli 21, Garth anaamini mbio za Salah za kutaka kuchukua Golden Boot kunasababisha asiweze kusaidia wachezaji wenzake kufunga magoli.

Hivi karibuni wachezaji wa Liverpool walidai kwamba wanasimamia na kusubiri muujiza ili waweze kuingia top 4 na kucheza ligi ya mabingwa ulaya na kufanya hivyo kutahitaji wachezaji wote kujitoa bila kuweka matakwa binafsi mbele.

Salah anapewa nafasi kubwa kwenye mbio hizi za kuwania Golden boot kwa kuwa wana michezo minne tofauti na Kane ambaye timu yake imebakiwa na michezo mitatu. Liverpool watashuka dimbani siku ya alhamis kuvaana na United ambao nao wanatafuta kila namna ya kumpora City nafasi ya kubeba taji la EPL.

PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Mbio, Mbio Za Golden Boot Za Salah Zazua Hoja, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa