Mchezo wa fainali ya CRDB Federation Cup kati ya Yanga SC vs Singida Black Stars umepelekwa mbele mpaka Juni 29 2025, Uwanja wa New Amaan saa 2:15 usiku.
Awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Juni 28 2025, mabadiliko hayo yametokana na uwepo wa mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya Yanga SC vs Simba SC.
Mtanange wa Kariakoo Dabi awali ulitarajiwa kuchezwa Juni 15 2025, umepelekwa mbele mpaka Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa kwa wababe hao kukutana kusaka pointi tatu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kusogezwa mbele kwa fainali hii ni kutoa muda wa kutosha wa kujiandaa kwa timu ya Yanga kwani watakua wamemaliza mchezo wa mwisho wa ligi siku mbili kabla.
Mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Yanga SC ilifika hatua ya fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Inakwenda kukutana na Singida Black Stars ambayo iliwafungashia virago Simba SC kwenye hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 3-1