Mckenna Aongeza Mkataba Ipswish

Kocha wa klabu ya Ipswich Town ambayo imepanda ligi kuu ya Uingereza Kieran Mckenna amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya hiyo kwa miaka kadhaa ijayo.

Mckenna ambaye amefanikiwa kuipandisha klabu hiyo madaraja mawili kutoka Ligue one kwenda Championship na sasa ligi kuu ya Uingereza amehakikishiwa ulaji ndani ya Ipswich Town kwa muda mrefu zaidi baada ya kazi kubwa aliyoifanya.mckennaKocha huyo amezungumza baada ya kusaini mkataba huo “Nina furaha sana kwa kuweka mustakabali wangu kwa hatua inayofuata na Ipswich Town na nina hamu kubwa ya kile kinachokuja tunaposonga mbele pamoja katika safari hii.”

Kocha huyo amekua akihusishwa na vilabu kadhaa vikubwa punde tu alipofanikiwa kuipandisha klabu ya Ipswich ligi kuu ya Uingereza, Inaelezwa vilabu vya Chelsea, Brighton, na Man United vilikua vikifukuzia saini yake lakini kwasasa ameamua kujifunga ndani ya klabu ya Ipswich.mckennaKocha Kieran Mckenna alikua anaelezwa anaweza kua mbadala wa kocha Erik Ten Hag ambaye mpaka sasa hatma yake haijafahamika ndani ya klabu hiyo, Hii inatokana na kua kocha huyo ameshawahi kufanya kazi ndani ya Man United chini ya Jose Mourinho na Ole Gunnar Solskjaer jambo ambalo lingekua jepesi lakini haijakua hivo na ameamua kusalia Ipswich Town.

Acha ujumbe