Jose Mourinho alitupiwa virago na Manchester United, lakini bado ana mahusiano mazuri na wachezaji wake wa zamani.

Penati ya Bruno Fernandes ilihihakikishia United pointi moja walipocheza dhidi ya Spurs Ijumaa usiku na lilikuwa goli la dakika za majeruhi.

Tofauti na Scott McTominay, ambaye alimkimbilia Mourinho na kwenda kumkubatia baada ya mechi.


Mourinho alimpandisha McTominay kutoka akademi alipokuwa kocha wa United na kumsaidia kumbadilisha kuendana na mfumo wa Red Devils.

McTominay amekuwa akiimarika sana tangu Mourinho alipotimuliwa mwishoni mwa 2018 na amecheza mara 28 msimu huu chini ya Ole Gunnar Solskjaer.

McTominay hajasahau namna Mourinho alivyomsaidia ni mmoja ya wachezaji walikwenda kumkumbatia kocha huyo wa Spurs.


41 MAONI

  1. Mc tominay ni mchezaji mwenye heshima kubwa na anakumbuka fadhila alizofanyiwa na jose mourinho,hii nzuri sana sio kwa tominay ila ningependa iwe kwa wachezaji wote man u maana nikocha ambaye aliyewafundisha pale old traford napia maelewano mazuri na kocha wanaweza kukutoa sehem kwenda nyingine safi mc tominay

  2. Jambo nzuri sana hilo mana amekumbuka wapi alipo toka na wapi yupo na ninani amemsaidia wapo watu wachache ambao huwa wanakumbuka sana fadhila asante sana meridian

  3. Ni jambo zr kulumbuka fadhila kwa mtu alie kutendea kuondoka kwake machon mwako sio sabab ya kuusahau utu wake kwako mc tominay anakumbuka alivyo tolewa academy mpk kwa wakubwa

  4. nzuri sana sio kwa tominay ila ningependa iwe kwa wachezaji wote man u maana nikocha ambaye aliyewafundisha pale old traford napia maelewano mazuri na kocha wanaweza kukutoa sehem kwenda nyingine safi mc tominay

  5. Ni vizuri kukumbuka fadhila kwa aina ya mchezaji Kama mc Tominay kukaba Sana anapokua dimbani ndio wachezaji wanao mvutia morinho

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa