Mctominay Njia Nyeupe kueleka Napoli

Kiungo wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Scotland Scott Mctominay yuko mbioni kujiunga na klabu ya Napoli kutoka nchini Italia.

Manchester United wamekubali dau la Euro milioni 30 ambayo imetolewa na klabu ya Napoli kwajili ya kupata huduma ya kiungo wao Mctominay, Hivo taratibu zingine zinakamilishwa kwajili ya kuhakikisha mchezaji huyo anajiunga na mabingwa hao wa Italia msimu miwili iliyopita.mctominayKiungo huyo alikua anahitajika na klabu ya Fulham ambapo klabu hiyo jijini London haikua tarari kulipa kiasi cha Euro mlioni 30, Napoli wao wamekubali kutoa kiasi hicho cha pesa na hatimae Man United wamekubaliana na klabu hiyo jambo ambalo linakwenda kumaliza safari ya muda mrefu kiungo huyo ndani ya jezi ya Man Unied.

Kocha wa klabu ya Napoli Antonio Conte ndio amependekeza jina la Scott Mctominay kua ni kiungo ambaye anataka kumuona kwenye timu yake katika msimu akiamini anaweza kuongeza kitu ndani ya kikosi hicho ambacho kimekua hakina mwendelezo mzuri tangu walipopata ubingwa msimu wa 2022/23.

Acha ujumbe