Mejbri Kuungana na Kikosi Kikubwa United.

Juhudi, maarifa na uvumilivu, ni vitu vikubwa kwenye maisha ya wanasoka. Hannibal Mejbri huenda akaona matunda ya sifa hizo kuelekea mwishoni mwa msimu huu.

Mejbri ni kijana wa miaka 19 ambaye anaitumikia Manchester United katika ngazi ya vijana (wachezaji chipukizi). Akiwa nacheza katika safu ya kiungo, wapo baadhi ya wadau wa soka wanaomuona Hannibal kama mbadala sahihi wa Paul Pogba.

Mejbri

Akiwa tayari ameitumikia Timu ya Taifa ya Tunisia kwa mara 11, Hannibal anarejea United baada ya Tunisia kuondolewa kwenye mashindano ya AFCON 2021. Kurejea kwake kunampa fursa ya kuonesha uwezo wake kwa kocha mpya wa klabu hiyo, Ralf Rangnick.

Rangnick hajawahi kumuona Mejbri kwenye mazoezi lakini, kwa taarifa fupi aliyonayo kuhusu mchezaji huyo, anaamini ni mchezaji sahihi kwenye timu yake na, atampatia nafasi ya kujiunga na wachezaji wakubwa kwa muda wa miezi 4 iliyosalia msimu huu.

Hii ni nafasi adhimu wa Hannibal ambaye, anapita njia walizopita Marcus Rashford, Mason Greenwood, Scot McTominay na Jesse Lingard ambao wote walikua kwenye timu ya wachezaji chipukizi.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.