Soka la kitaa linanendelea kuwa fursa kwa vijana na kuwa chachu ya ushirikiano, Meridianbet Mkuchu Cup imechukua taswira hii kwa vijana kutoka maeneo mbali mbali ya kata ya Kunduchi na sehemu mbali mbali za Dar es salaam.

Meridianbet Mkuchu Cup ilianza kwa kushirikisha jumla ya timu 20 kutoka maeneo ya Mwananyamala, Mwenge, Kinondoni, Magomeni, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Kawe, Mabwepande na Msasani katika dimba la Machava.

Lengo la michuano hii ambayo imemaliza ngazi ya robo fainali wikiendi iliyopita ilikuwa ni kutoa fursa kwa vijana kuweza kuonesha vipaji vyao. Pia, michuano ya Meridianbet Mkuchu Cup ilikuwa ni fursa ya vijana kupata ajira kwa kulipwa kuwakilisha timu zinazoshiriki, na ilikuwa fursa ya kuwakutanisha vijana na kuchchea umoja baina yao.

MERIDIANBET MKUCHU CUP
Mchezaji bora wa Mianzini FC akikabidhiwa zawadi na John Mwakalosi kutoka Meridianbet.

“Vijana ni nguvu kazi ya taifa, na wana vipaji sana lakini baadhi yao bado hawajaonekana vyema kwenye tasnia ya soka, michuano hii inawapa nafasi ya kuonekana kwa jamii na kujipatia fursa ya ajira, pia hii ni burudani kwa wananchi wanaohudhuria michuano hii.” Alizungumza Emmanuel Mkuchu, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kilongawima, ambaye ni mratibu wa michuano hii kwa kushirikiana na Meridianbet.

Wikiendi hii mechi za robo fainali za ligi ya Meridianbet Mkuchu cup zimemalizika na kutoa washindi wanaosonga hatua inayofuata. Kwenye robo fainali, Mabwe Young Boys waliwachakaza Mtongani Famili goli 3 – 0, huku Nondo FC wakiwachapa Kilongawima Boys 2 – 0, wakiungana na Tanga Boys pamoja na Mianzini ya Magomeni kuelekea Nusu Fainali.

Kwa upande wa Meridianbet, ambao ni wadhamini wa michuano hii kupitia Twaha Mohamed anayetokea kitengo cha masoko cha kampuni hiyo, wanasema hii ni sehemu yao ya shughuli ya kurejesha kwa jamii na kutoa fursa kwa vijana.

“Vijana wanaonesha uwezo mkubwa sana hapa, sisi kwetu huu ni muendelezo wa jitihada zetu za kushirikiana na jamii, tukiwa tunarejesha kwa jamii tunayoshirikiana nayo kila siku.”

Nusu fainali ya michuano hii inayotarajiwa inatarajiwa kuchezwa Februari 11 na 12 na kurudiwa Februari 18 na 19 na kisha fainali ikipangwa kuchezwa Februari 26. Bila shaka ungependa kujionea burudani ya soka na vipaji kutoka mtaani kupitia Meridianbet Mkuchu Cup.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa