Mchezaji nyota wa Argentina Lionel Messi amesema kuwa anaamini kuwa anaanza kuendana na Psg baada ya kuhitaji mwaka mmoja kutulia mara baada ya kuhamia Ufaransa.
Messi alifunga mabao 11 pekee katika mechi 34 msimu wake wa kwanza Psg mnamo 2021/2022, lakini tayari amefunga mabao sita katika mechi 11 za miamba hao wa Ligue 1 katika kampeni yao ya msimu huu.
Mchezaji huyo wa zamani wa FC Barcelona pia anafurahia kiwango chake cha Kimataifa akifunga mara mbili na kutoa assist huku Argentina ikiendeleza msururu wao wa kutopoteza hadi mechi 34 kwa ushindi wa 3-0 wa kirafiki dhidi ya Honduras siku ya Ijumaa.
Akizungumza na TYC Sports baada ya ushindi huo Messi alilinganisha kiwango chake cha sasa na cha msimu uliopita. “Ninajisikia vizuri, tofauti na mwaka jana na nilijua itakuwa hivyo” Messi alisema.
Mwaka jana alikuwa na wakati mbaya na alishindwa kujipata kabisa ambapo licha ya hayo yote alikuwa anapata nafasi katika klabu yake. Mchezaji huyo anasema kuwa yeye ni mmoja wa watu wanaoamini kuwa mambo yanatokea kwasababu, na Mungu ndiye hupanga yote.
Lakini sasa anafurahia na kila wakati wanajiandaa kwa umakini azid kufanya kazi. Kwahiyo wanachukua fursa hiyo kuendelea kukuza kile wanachojua na kujaribu vitu vipya pia”.