Mchezaji wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi anafurahia kujiunga tena na rafiki wake wa zamani Neymar katika klabu hiyo baada ya kutengana kwa miaka kadhaa.

Messi amepata furaha kujiunga tena na nyota mwenzake wa zamani wa klabu ya Barcelona ambaye walitengeneza ushirikiano sana klabuni hapo kwa miaka waliyoishi pamoja ndani ya timu hiyo pamoja na kushinda mataji tofauti tofauti.

messiMessi na Neymar wamefanikiwa kushinda mataji kadhaa wakiwa katika klabu ya Barcelona kama La liga,Copa de Le Rey,ligi ya mabingwa barani ulaya na mataji mengine kabla ya klabu ya PSG kuvunja rekodi ya usajili na kumchukua mchezaji huyo kumpeleka nchini ufaransa kuwatumikia matajiri hao.

Tatizo la kiuchumi ndani ya klabu ya Barcelona iliwafanya jklabu ya Barca kulazimika kumuachia mchezaji wao Lionel Messi kujiunga PSG mwaka 2021 na kwenda kuwakutanisha marafiki hao wa zamani kitu.

Wakiwa wameanza msimu huu kwenye ubora mkubwa huku kwa pqmoja wakiwa wameshiriki magoli 19 ndani ya klabu hiyo kuliko wachezaji wote katika ligi bora tano ulaya.

“Neymar tumefahamiana muda mrefu,kwa moyo wangu ningetamani kuendelea kumfurahia zaidi akiwa Barca”Lakini sasa tunakutana tena PSG nina furaha kucheza naye”Alisema Messi

Messi na Neymar ni marafiki wanaopendana na kuheshemiana kwa kila anachokifanya mwenzake na hii imejenga upendo mkubwa baina ya wachezaji hao wawili nguli.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa