Messi, Baada ya Ubingwa ni Likizo!

Lionel Messi amefanikiwa kutimiza ndoto yake. Nahodha huyo wa Argentina aliongoza nchi yake kutwaa taji lao la kwanza tangu 1993 Jumamosi usiku, wakiifunga Brazil 1-0 katika fainali ya Copa America huko Maracana, Rio de Janeiro.

Messi leo ataenda likizo na familia yake, na maisha yake ya baadaye baada ya likizo bado hayana uhakika. Muargentina huyo, kwa mujibu wa Mundo Deportivo, ataenda kwenye mapumziko ya wiki tatu, lakini kwa sasa ipo wazi kuwa ni wakala huru baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa Barcelona.

Messi Copa America 2021
Messi Copa America 2021

Mkataba wake na Barcelona ulimalizika mnamo Juni 30, na licha ya nia ya pande zote mbili kuongeza mkataba, suala la mshahara ulioamriwa na La Liga limekuwa gumu. Mazungumzo bado yanaendelea, lakini haionekani kama Barcelona watatangaza karibu kama ilivyokuwa wiki chache zilizopita.

Barcelona, wakiongozwa na Joan Laporta, wanafanya kila wawezalo kupunguza mshahara wao. Hii inamaanisha kuhamisha wachezaji waziada kadri iwezekanavyo na kisha kuhamia kwa wenye kipato cha juu.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

Acha ujumbe