Staa wa klabu ya Inter Miami na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amesema kua wachezaji nyota Kylian Mbappe wa PSG na Earling Haaland wa klabu ya Manchester City watashinda Ballon Dor siku moja.
Messi amesema hayo katika hafla ya utoaji wa tuzo za Ballon Dor jijini Paris usiku wa jana, Ambapo staa huyo alitwaa tuzo yake ya Ballon Dor ya nane katika hafla hiyo.Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina wakati akizungumza jana baada ya kukabidhiwa tuzo yake ya nane ya Ballon Dor aliweka wazi kua wachezaji Mbappe na Haaland wana nafasi kubwa ya kuja kutwaa tuzo hiyo siku za mbeleni.
Mshambuliaji Earling Haaland alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika tuzo hizo baada ya mshindi wa kombe la dunia nchini Qatar, Huku Mbappe akikamata nafasi ya tatu na ndio sababu ya gwiji huyo kuona vijana hao watakuja kutwaa tuzo hiyo siku za mbeleni.Mshambuliaji Lionel Messi jana alifanikiwa kutwaa tuzo yake ya nane ikiwa ni wazi anakua mchezaji aliatwaa tuzo ya Ballon Dor mara nyingi zaidi, Huku akimzidi mshindani wake karibu Cristiano Ronaldo tuzo tatu mpaka sasa.