Miaka Siyo Shida, Wakongwe Wanaoendeleza Ubabe

Imezoeleka kwamba mara nyingi mchezaji anapofika miaka kuanzia 30 uwezo wake wa kisoka na kucheza mpira wa ushindani hupungua pia kwa kiwango fulani; na maisha yake kisoka kwa wakati huo yanaikuwa yanaelekea kwenye ustaafu. Pamoja na hilo wachezaji wengi wamekuwa wakifanya tofauti wanapokuwa katika umri huo kwa kuonekana bado wanatoa mchango mkubwa katika vikosi vyao.

Kwa wachezaji kama Ronaldo ambaye ana umri wa miaka zaidi ya 30 kwa sasa, anaonekana bado yupo kwenye hali ya kiushindani sana ambayo inaweza kulinganishwa na kijana wa miaka 25, pia kwa Messi ambaye anasogea naye akiwa na miaka zaidi ya 30 kwa sasa anaonekana bado ana upekee mkubwa wa kuendeleza katika soka kwa sasa na hata baadae.

Kuna wakati tunaamini kwamba umri ni namba tu kutokana na haya yanayofanywa na hawa wachezaji ambao tayari wamevuka umri huo wa miaka hiyo 30 inayohisiwa kuwa viwango vingi huanza kudumaa taratibu. Wachezaji wengine ni kama:

Dani Alves

Raia huyo wa Brazil alikuwa kiraka ndani ya kikosi cha Tuchel kwa kuonesha thamani yake tangia asajiliwe kutoka Barcelona. Pamoja na kukumbwa na majeraha na kumfanya kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu lakini bado amerejea kwenye ubora wake. Umri wake wa miaka 35 siyo kitu kwake kwa wakati huu kwenye soka lake.

Bruno Alves

Raia huyo wa Ureno alikuwa msaada wa kutosha ndani ya timu ya taifa na klabu yake iliyopanda daraja katika ligi ya Italia, Serie A. Bado anastahili pongezi kwa kile kikubwa alichokifanya kuisadia timu yake kuendelea kujihakikishia nafasi ya kuendelea kusalia jwenye ligi kuu. Umri wake kwa sasa ni miaka 38 ambayo mingi kwa mchezaji anayecheza soka la ushindani.

Joaquin

Raia huyo wa Hispania aliyekipiga katika klabu ya Real Betis hakuonesha dalili yoyote ya kushuka kwa kiwango chake ndani ya kikosi hicho na aliendelea kutoa msaada ndani ya kikosi chake pamoja na umri wake kusogea sana. Pamoja na kuwa na umri wa miaka 38 bado alikuwa nguzo kubwa katika eneo la kiungo la kikosi hicho.

Franck Ribery

Miongoni mwa tunu ambazo Bayern Munich walijivunia ni kuwa na mchezaji wa aina yake, ambaye amefanya kila lililo kubwa ndani ya kikosi chao. Ameshiriki mashindano makubwa mengi na kuchukua vikombe vingi lakini hadi sasa uwezo wake bado haujashuka anaendelea kufanya vizuri zaidi.

2 Komentara

    Nikweli hizo ni nambatu chamsingi hapo nikuona kama anaweza kucheza vizuri akiwa uwanjani#meridianbetz

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe