Hali bado ni tete katika klabu ya Arsenal, kupoteza michezo imekuwa ni sehemu ya matokeo yao. Mikel Arteta anawalaumu wachezaji wake nyota katika kikosi hicho.

Mchezo dhidi ya Tottenham Hotspurs umedhihirisha ni kiasi gani, Arsenal hainasumu katika mashambulizi yao.

Licha ya vijana wa Mikel Arteta kuutawala mchezo kwa 69.2%, ni Lacazette pekee aliyejitahidi na kupiga mikwaju miwili iliyolenga goli. Hakuna mchezaji mwingine yeyote wa Arsenal aliyefanya hivyo.

Mikel Arteta, Mikel Arteta Anawalaumu Nyota Wake., Meridianbet
Aubameyang (kushoto) akianzisha mpira na Lacazette (katikati) baada ya kufungwa na Tottenham.

Huu ni msimu ambao safu ya ushambuliaji ya Arsenal kwa pamoja (Aubameyang na Lacazette) wanamagoli 5 tu! Ikilinganishwa na wapinzani wao (Kane na Son) ambao kwa pamoja wanamagoli 18 na pasi 13 za magoli.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Arteta amesema ” Ukiangalia takwimu zote zipo upande wetu, lakini mwisho wa siku suala ni kufunga magoli. Tulikuwa na nafasi, pengine tumetengeneza nafasi nyingi zaidi [kwenye mchezo huu] kwenye msimu huu.

Mikel Arteta, Mikel Arteta Anawalaumu Nyota Wake., Meridianbet
Harry Kane akishangilia goli na Son Hueng-Min

“Lakini mwisho wa siku tunapaswa kufunga magoli, wao [Tottenham] hata walipopata nafasi kidogo, walifunga magoli lakini kwa sasa hatufungi. Ili kujenga kitu, unahitaji matokeo.

“Kuna vitu vingi nimevipenda kwa namna tulivyocheza, kujiamini, nguvu, na kujitambua ni vitu vizuri. Mwisho wa siku ni mchezo wa soka na unatakiwa kushinda, lakini tumefungwa tena leo.”

Mikel Arteta anakwama wapi?


MALIZA MWAKA KIBINGWA KWA KUJISHINDIA SHEA YAKO KWENYE SHILINGI 140,000,000TSH!!

Kipindi hiki cha sikukuu kinamalizika kwa namna ya kipekee. Shilingi 140,000,000 kushindaniwa katika michezo ya Evolution kwenye Kasino Mubashara ya Meridanbet. Ingia mchezoni na ujiwekee nafasi ya kushinda shea yako!!!

Mikel Arteta, Mikel Arteta Anawalaumu Nyota Wake., Meridianbet

SOMA ZAIDI

23 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa