Arsenal hawana mpango wa haraka wa kumtimua kocha mkuu Mikel Arteta kabla ya kuanza kwa msimu ujao.

Shinikizo sasa linaanza kuongezeka kwa Arteta, kufuatia timu yake kutofuzu nusu fainali ya Ligi ya Uropa dhidi ya Villarreal Alhamisi usiku.

Washika bunduki walipata sare ya bila kufungana huko Emirates, ambayo ilitosha kuona wana La Liga – waliowahi kusimamiwa na bosi wa zamani Unai Emery – kusonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1.

Kwa mujibu wa Daily Mail, uongozi wa Arsenal hauamini kuwa mabadiliko ya meneja ni muhimu wakati huu, hasa baada ya kampeni isiyo kawaida ya 2020-2 iliyoathiriwa na coronavirus

Arteta.

Hata hivyo, bodi ya Gunners imesikitishwa kwamba klabu haijafanya kwa kiwango kinachotarajiwa muhula huu na wanatarajia maboresho makubwa msimu ujao.

Ikiwa Arteta atabaki na kuwajibika zaidi ya kampeni hii, mwanzo mbaya wa msimu wa 2021-22 utaweka hatiani kibarua cha meneja huyu wa miaka 39.

Mmiliki wa Arsenal, Stan Kroenke, ambaye anasisitiza kuwa klabu haiuzwi, atahakikisha kuna fedha zinazopatikana kwa msimu ujao, lakini mipango yao ya kusajili inategemea sana iwapo Gunners wanaweza kupata kufuzu kwa Uropa


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Arteta, Mikel Arteta Bado Ana Nafasi Arsenal, Meridianbet

SOMA ZAIDI

11 MAONI

  1. Kwa mujibu wa Daily Mail, uongozi wa Arsenal hauamini kuwa mabadiliko ya meneja ni muhimu wakati huu, hasa baada ya kampeni isiyo kawaida ya 2020-2 iliyoathiriwa na coronavirus

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa