Ghala la silaha jijini London la washika mitutu wa Arsenal, linateketea chini ya utawala wa Mikel Arteta.

Arsenal wanaendelea kupata matokeo mabaya tangu walipopata ushindi dhidi ya Man United katika dimba la Old Trafford.

Kipigo dhidi ya Wolves (2-1) kinaendelea kuhatarisha maisha ya Arteta ndani ya kikosi hicho ambacho hakionekani kikirejea kwenye ubora wake kwa siku za karibuni.

Mikel Arteta amekiri mfululizo wa matokeo mabaya ikiwa ni pamoja na kupoteza michezo, kunashusha sana uwezo wa kujiamini kwa wachezaji wake.

Mikel Arteta, Mikel Arteta “Vipigo Vinaathiri Kujiamini”., Meridianbet
Aubameyang baada ya mchezo dhidi ya Wolves (2-1).

Akizungumza na BBC Sports baada ya mchezo dhidi ya Wolves, Arteta amesema ” [Wolves] walipiga mashuti mawili yaliyolenga goli na walifunga. Timu ilionesha uwezo wa kustahimili, umoja na imani ya kutafuta ushindi kwenye kipindi cha pili. Tulitengeneza nafasi lakini hatukufunga.

“Tunahitaji magoli mengi ili tupate ushindi.Tunapaswa kuwapa nguvu wachezaji, kila mchezaji anapitia kipindi kigumu. Tunatengeneza nafasi lakini tunashindwa kufunga magoli. Hiyo ndio tofauti kati ya kushinda na kushindwa.

Mikel Arteta, Mikel Arteta “Vipigo Vinaathiri Kujiamini”., Meridianbet
Daniel Podence akishangilia goli lililowapa ushindi Wolves dhidi ya Arsenal.

“Unapopoteza mchezo, uwezo wa kujiamini unashuka kwasababu [wachezaji] wanaamini kitu hicho kitatokea tena.

“Unahitaji ushindi baada ya kufungwa. Ndivyo tulivyokuwa tunafanya wakati nilipokuwa hapa. Hii ni mara ya kwanza tangu tumekuwa hapa [kupoteza michezo mfululizo]”

Arsenal wanapoteza mchezo wa 3 mfululizo wakiwa nyumbani, wameshinda mchezo 1 kati ya 6 waliyocheza kwa siku za karibuni na sasa wanashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa EPL.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Mikel Arteta, Mikel Arteta “Vipigo Vinaathiri Kujiamini”., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa