Klabu ya AC Milan inaripotiwa kuwa haina mpango wa kumuuza nyota wake Alessio Romagnoli katika msimu huu wa uhamisho wa kiangazi.
Kapteni huyu amekuwa na changamoto ya mda wa kucheza klabuni hapo katika wiki za hivi karibuni, na beki huyu amekuwa akiwekwa benchi na Stefano Pioli.
Milan wanatarajiwa kuchukua uamuzi wa kumnunua Fikayo Tomori kutoka Chelsea kwa dau la €28m na ripoti huko Italia zinataja kuwa biashara ya kumuuza Romagnoli ingeweza kufadhili kumnunua Tomori.
Lakini kwa mujibu wa La Gazetta delo Sport, staa huyu mweye miaka 26, ambaye ameichezea Italia mara 12, yupo tayari kupambania nafasi yake Milan.
Milan wapo nafasi ya tatu kwenye Ligi, na kama watafuzu kuingia ligi kuu basi watahitaji kuwa na mabeki wa kati wakubwa angalau watatu.
Hivyo, suala la kufikiria kumuuza Romagnoli linaonekana kutokuwepo kwenye karata ambazo wanataka kuzicheza, kwa mujibu wa chaoisho hilo.
Romagnoli amecheza mechi 22 za Serie A msimu huu na ripoti zinasema kuwa yupo tayari kuendelea kupambania nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Mwacheni ni mchezaji mzuri
Asnte kwa taarfa
Asanteni kwa makala
Sawa
Tumeelewa
Habar njema
Tumeelewa
Ni jambo zuli
Safiii
Safii