Klabu ya AC Milan yaendeleza ubabe wake huko Serie A ambapo mpaka sasa hajapoteza mchezo wowote katika mechi sita alizocheza. Milan ameweza kushinda mchezo wa jana ugenini dhidi ya Sampdoria licha ya kupata kadi nyekundu.

 

Milan Kuendeleza Ubabe

Mabingwa hao watetezi walitawala mchezo katika kipindi cha kwanza ambapo mpaka walipoenda mapumziko walikuwa wakiongoza kwa bao moja kwa bila, goli ambalo lilifungwa na Junior Messias ambalo ndilo bao lake la kwanza msimu huu.

AC Milan walistahili kadi nyekundu ya Raphael Leao kipindi cha pili baada ya kupata kadi ya njano ya pili kutokana na kucheza madhambi na hivyo kuwafanya Sampdoria waweze kusawazisha bao hivyo kuwa moja kwa moja kupitia kwa mchezaji wao Filipo Djuricic muda mfupi kabla ya saa moja kuisha.

 

Milan Kuendeleza Ubabe

Licha ya kuwa kupata kadi nyekundu na Milan kubaki na wachezaji kumi uwanjani dakika ya 67 wanapata penati ambayo imetokana na mchezaji wa Sampdoria kuudaka mpira katika eneo la hatari hivyo kufanya ubao wa matokeo usomeke Sampdoria 1-2 AC Milan ambapo mkwaju huo wa penati ulipigwa na Olivier Giroud

Kutokana na ushindi huo walioupata vijana wa Stefano Pioli kwenye msimamo wapo sawa na Napoli kwenye msimamo ambapo tofauti kati yao ni mabao yakufungwa na kufunga, Wakati huo huo Samdoria wamevuna alama mbili tuu toka ligi ianze kitu ambacho ni ishara mbaya kwao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa