Milan Kuzungumza Dili la Fikayo Tomori

Boss wa AC Milan Paolo Maldini amethibitisha kwamba Rossoneri wanataka kuzungumzia dili la kudumu la FikaTomori na klabu yake mama ya Chelsea.

Tomori alikuwa anapata wakati mchache wa kucheza chini ya meneja wa zamani wa The Blues Frank Lampard na alielekea San Siro kwa mkopo mnamo Januari, ambapo ameonekana kuwashawishi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amecheza dakika 90 kwenye mechi tatu Serie A hadi sasa – ikiwa ni pamoja na ushindi wa Jumapili wa 2-1 dhidi ya Roma – lakini mkurugenzi wa klabu Maldini anataka kupandisha bei ya nyota huyo wa Chelsea ya pauni milioni 26 kabla ya kuanza kufanyia kazi kifungu cha kumnunua.

Fikayo Tomori

Akiongea na Sky Sports Italia, Milan wanasema: “Tomori ni mchezaji ambaye ana sifa za kasi na ukali na kwetu, alikuwa mtu wa kuimarisha.”

“Tomori ni talanta nzuri na tuna kifungu cha chaguo la kumnunua. Bei ni kubwa sana. AC Milan itaamua mwishoni mwa msimu huu na tutaijadili na bodi ya Chelsea.”

Tomori pia amejitokeza katika Ligi ya Uropa na Coppa Italia kwa kikosi cha Stefano Pioli, ambao wanakaa alama saba nyuma ya vinara Inter Milan wakiwa na mchezo mkononi.


Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx

Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.

  CHEZA HAPA

8 Komentara

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Tomori anajua sema hajapata nafasi

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Wampe nafasi aonyeshe maajabu yake

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Milan mchukuen

    Jibu

    Jambo zur

    Jibu

Acha ujumbe