Klabu ya AC Milan imeripotiwa kuanza mazungumzo na nyota wake Frank Kessie kwa ajili ya makubaliano ya mkataba mpya.

Nyota huyu ambaye ni raia wa Ivory Coast ameweza kuwa sehemu muhimu ya Kikosi cha Pioli pale San Siro wakati mkataba wake wa sasa ukifika tamati Juni 2022.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari za michezo, Milan sasa wanafanya kazi mazungumzo ya wachezaji wao watatu ambao mikataba yao inakaribia kuisha.

Wachezaji ambao wanatajwa kuwa mazungumzo juu ya hatma ya mikataba yao mipya yanaendelea ni pamoja na Zlatan Ibrahimovic, Gianluigi Donnarumman na Hakan Calhanoglu.

AC Milan Frank Kessie

Hata hivyo, kwa mujibu wa La Gazzeta dello Sport, klabu hii imeanza mazungumzo na Kessie pia.

Kessie ameshiriki katika mechi 9 Milan msimu huu wa Serie A. Amefanikiwa kupata magoli matatu na asisti 2 mpaka sasa.

Nyota huyu anaweza kufikisha idadi ya mechi zake 150 kwa klabu hiyo dhidi ya Celtic Alhamisi hii. Anaikamilisha idadi hii kwa mda wote aliyokuwepo klabuni hapo tangia alipotua kutoka Atalanta mwaka 2017.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Milan, Milan: Mazungumzo Mkataba Mpya wa Frank Kessie, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa