Milan Skriniar beki huyo wa Inter Milan ya nchini Italia ataendelea kusalia klabuni hapo kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya soka nchini Italia.

Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Giussepe Marotta ameeleza beki huyo wa kimataifa wa Slovakia ataendelea kubakia ndani ya Inter Milan licha ya vilabu kadhaa kuwinda saini ya beki huyo wa kati ambae ni miongoni mwa nguzo za klabu hiyo kwenye eneo la ulinzi akishirikiana na mabeki wengine kama Alexandro Bastoni,Fedrico Dimarco, pamoja na Stefan De Vrij chini ya mwalimu wa Simeone Inzaghi.

milan skriniar, Milan Skriniar kusalia ndani ya Inter Milan., Meridianbet

Klabu ya Paris saint German ni klabu ya ambayo ilikua inamfatlia kwa karibu sana Milan Skriniar kumuhitaji akaongeze nguvu kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Lakini msimamo wa klabu ya Inter Milan ni kua beki hauzwi na ataendelela kusalia klanuni hapo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa