Milan Waanza Mazungumzo na Lucas Vazquez

Milan wanaripotiwa kuwa tayari wameanza kufanya mazungumzo ya kumsajili winga wa Madrid Lucas Vazquez kama mchezaji huru.

Klabu hii inakumbana na upinzani wa kuiwania saini hiyo kutoka kwa vilabu vya Inter Milan, Bayern Munich na Manchester United.

Kwa mujibu wa Calciomercato, mkurugenzi wa ufundi wa Milan, Paolo Maldini tayari ameshawasiliana na uwakilishi wa mchezaji huyo, licha ya kipaumbele cha nyota huyo wa hispania kuwa ni kuendelea kusalia Real Madrid.

 Lucas Vazquez
Lucas Vazquez

Uwakilishi wa Vazquez umedai kuhitaji mkataba mpya wa miaka minne, wenye thamani ya euro milioni 5 kwa mwaka, lakini taarifa zinataja kuwa si Real Madrid wenyewe au Milan ambao wapo tayari kwa masharti hayo.

Milan wao kwa upande wao wanaweza kumpa mkataba wa mwaka wa euro milioni 4, ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi wanachoweza kumlipa mchezaji ukiachana na Zlatan Ibrahimovic na Gigio Donnarumma.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

2 Komentara

    Inapendeza

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

Acha ujumbe