Milan Wanapaswa Kupambana na Vilabu vya EPL Kumpata Fofana

Milan wako tayari kuzindua mpango madhubuti wa kumnunua Youssouf Fofana lakini watalazimika kupigana na Paris Saint-Germain na vilabu vingi vya Ligi Kuu ya Uingereza kumnunua kiungo huyo wa Monaco.

Milan Wanapaswa Kupambana na Vilabu vya EPL Kumpata Fofana

Mipango ya The Rossoneri inaanza kupamba moto wakati dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi linakaribia kwa kasi, tayari kuanza kufanya harakati kabla ya msimu wa 2024-25. Ingawa kipaumbele chao ni mshambuliaji mpya wa kati kuongoza mstari wa mbele, klabu pia inatazamia kuimarisha maeneo mengine ya kikosi.

Milan wanataka kumchukua kiungo mkabaji mpya na pia wameanza kumlenga beki mpya wa kulia. Wakati huohuo, klabu hiyo imeanzisha rasmi kikosi chao kipya cha vijana chini ya umri wa miaka 23 huku wakipania kuiga mafanikio waliyoyaona Juventus na kikosi chao cha Next Gen.

Milan Wanapaswa Kupambana na Vilabu vya EPL Kumpata Fofana

Corriere dello Sport inaangazia jinsi mkurugenzi wa Milan Geoffrey Moncada yuko tayari kuingia katika mazungumzo mazito na Monaco ili kujaribu kumaliza dili la Fofana, ambaye bei yake ni ya karibu €20-25m.

Vilabu kadhaa pia vina nia ya kumnasa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 25, ikiwa ni pamoja na PSG na baadhi ya vilabu vya Premier League vikiwemo Tottenham na Liverpool.

Acha ujumbe