Nyota wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovicameripotiwa kuwepo kwenye mawasiliano na mtaalamu juu ya matibabu yake ya goti.Taarifa zinasema staa huyu anajaribu kufanya tahmini kama aendelee na matibabu ya kawaida au afanyiwe upasuaji.

Nyota huyu mwenye miaka 39, alipata jeraha la goti wiki iliyopita kwenye mechi dhidi ya Juventus .

Licha ya meneja Stefano Pioli kuweka wazi kuwa staa huyu atapona taratibu kadri mda unavyokwenda na kurejea dimbani, baadhi ya vyanzo nchini Italia vinasema kuwa nyota huyu hataweza kurejea tena dimbani msimu huu.

Zlatan Ibrahimovic

Kwa mujibu wa La Gazzetta dello Sport, ZLatan anafanya mawasiliano na mtaalamu wa goti, Profesa Volker Musahl huko Pittsburgh kwa ajili ya kutambua hali ya jeraha lake na uwezekano wa kupona bila upasuaji.

Profesa Volker Musahl ndiye mtaalami ambauye pia alimfanyia upasuaji staa huyu mwaka 2-17 alipokuwa akichezea Manchester United.

Zlatan tayari ameshasaini nyongeza ya mkataba wake, na anahitajika kuchagua njia ambayo itafaa kwa matibabu yake. Lakini ikiwa ataamua kufanyiwa upasuaji basi kunaweza kuwa na athari katika mwanzo wake wa msimu mpya, na pia ataikosa michuano ya Euro.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Zlatan, Milan: Zlatan Ibrahimovic Atafanyiwa Upasuaji?, Meridianbet

CHEZA HAPA

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa