Ripoti zinasema mabosi wa Manchester United wanamtazamia golikipa wa Roma, Mile Svilar kama mbadala wa Andre Onana baada ya mwenendo usioridhisha wa Mcameroon huyo aliyesajiliwa misimu miwili iliyopita akitokea Inter Milan.

Roma wanahitaji dau la euro milioni 50 ili kumuachia golikipa huyo amabaye amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake. Manchester United walimsajili Andre Onana kipindi cha kocha Eric Ten Hag kwa dau kubwa la euro milioni 50 lakini hajawapa kile walichokitegemea mashetani wekundu.
Onana amekua na msimu mbovu sana huku toka ajiunge na Manchester amefanikiwa kucheza michezo rasmi ya ligi kuu 72 akiruhusu kufungwa jumla ya mabao 102. Amepata ushindi mara 28 akipoteza mara 29, na kwa msimu huu pekee ameruhusu magoli 44 kwenye michezo 36 aliyoshiriki kwa upande wa ligi kuu.
Mbali na Manchester United, Bayern Munich, Manchester City, Chelsea, Newcastle, na Monaco pia wanatazama uwezekano wa kuipata huduma ya golikipa huyo ambaye mpaka sasa bado hajakubali kufanya mazungumzo ya kuboresha mkataba wake kwa muda uliosalia na Roma.



