Miloud Hamdi Atimkia Misri

Miloud Hamdi (54) raia wa Algeria, aliyekuwa kocha mkuu wa Klabu ya Yanga  ya Tanzania, ameteuliwa rasmi kuwa kocha mkuu wa Klabu ya Ismaily SC ya Misri kwa mkataba wa mwaka mmoja, ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi endapo pande zote zitakubaliana.

Miloud Hamdi Atimkia Misri

Miloud Hamdi anajiunga na Ismaily akitokea Yanga , ambako aliandika historia ya kipekee kwa kuiwezesha klabu hiyo kutwaa mataji matatu makubwa katika msimu wa 2024/2025. Chini ya uongozi wake, Yanga ilinyakua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho la CRDB (FA Cup), na Kombe la Muungano.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kuteuliwa kwa Miloud Hamdi kunakuja wakati Ismaily SC ikisaka kurejesha heshima yake katika soka la Misri, ikiwa ni mojawapo ya vilabu vyenye historia ndefu na mafanikio ya muda mrefu katika bara la Afrika.

Miloud Hamdi Atimkia Misri

Hatua hiyo pia inaashiria mwanzo mpya kwa Yanga , ambayo sasa italazimika kusaka kocha mpya atakayeendeleza mafanikio na ramani ya ushindani kimataifa ambayo Hamdi ameijenga.

Kocha huyo mwenye uzoefu, ambaye amewahi pia kuzinoa klabu kadhaa barani Afrika na Asia, anatarajiwa kuanza kazi mara moja akiungana na kikosi cha Ismaily kujiandaa kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Misri.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.