Ni muendelezo wa mabadiliko makubwa ndani na nje ya uwanja kule Manchester United. Paul Mitchell anapigiwa pande la kupata kibarua Old Trafford.

Mitchell ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa ufundi kule AS Monaco, huenda akatua kwenye viunga vya Manchester United kabla ya dirisha kubwa la usajili wa wachezaji kufunguliwa.

Anasifika kwa uwezo wake kwenye idara ya usajili  wa wachezaji na ameshafanya kazi hiyo na vilabu kadhaa ikiwemo Southampton na Tottenham kule nchini Uingereza. Sio nchini Uingereza pekee, pia amefanya kazi na RB Leipzig nchini Ujerumani na, ni miongoni mwa watu makini waliohusika kwenye maboresho ya mfumo mzima wa Leipzig inayotamba sasa hivi barani Ulaya.

Mitchell, Mitchell Apigiwa Pande United, Meridianbet

United ipo kwenye mchakato wa mabadiliko kuanzia kwa wachezaji, benchi la ufundi mpaka uongozi wa klabu. Ujio wa Erik Ten Hag kama kocha mkuu, akitegemewa kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Ralf Rangnick kama mshauri wa bodi, unatajwa kumueka mbele Paul katika nafasi ya kuiongoza idara ya usajili na ufatiliaji wa wachezaji.

Japokuwa Rangnick na Ten Hag wanapigia pande Mitchell, inasadikika baadhi ya viongozi wa United wanapinga ujio wa mtaalamu huyo wa ufundi hasa wakati huu ambao, Darren Fletcher ndiye anayeshikilia nafasi hiyo.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa