Mitrovic Aibukia Al-Hilal

Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Fulham United Aleksandar Mitrovic amefanikiwa kukamilisha dili lake na klabu ya Al-Hilal inayoshiriki ligi kuu nchini Saudia Arabia.

Mitrovic amekubali kujiunga na klabu ya Al-Hilal kwa dili la mkataba wa miaka mitatu ambapo klabu ya Fulham imefanikiwa kupokea zaidi ya kiasi cha Euro milioni 50 kutoka kwa klabu hiyo kutoka nchini Saudia.MitrovicKumekua na mvutano baina ya Al-Hilal na mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Serbia, Lakini mwisho dili limeonekana kutiki kutokana na makubaliano ya pande zote mbili baina ya mchezaji huyo na klabu ya Al-Hilal.

Klabu ya Fulham bado inakabiliwa na presha ya vilabu kutoka Saudia ambavyo bado vinahitaji wachezaji kutoka klabuni kwao, Kwani licha ya kumuongezea mkataba winga wa kimataifa wa Brazil Willian lakini bado anahitajika.MitrovicMshambuliaji Mitrovic anaongeza orodha ya wachezaji mbalimbali kutoka barani ulaya ambao wamejiunga na ligi kuu nchini Saudia Arabia maarufu kama Saudi Pro League ambapo maslahi makubwa yakitajwa zaidi kama kama sehemu ya ushawishi.

Acha ujumbe