Mkataba wa Kylian Mbappe Uliandaliwa Mara 7 Madrid!

Klabu ya Real Madrid inaripotiwa kuwa imeandaa mikataba mingi kwa kipindi cha mwezi uliopita ili kumvutia Kylian Mbappe. Mikataba inayoripotiwa kuandaliwa imefikia saba.

Real Madrid walikuwa tayari kulipa €220m (£188.56m) kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho la msimu wa joto ili kumnasa staa uyu wa Paris Saint Germain.

Hata hivyo, PSG wao hawakutaka kujibu ofa ya Real Madrid kumruhusu Mbappe aondoke, na mpaka sasa wapo kwenye hatari ya kumpoteza bure mwaka ujao, ikiwa hataongeza mkataba kusalia PSG.

Mkataba wa Kylian Mbappe Uliandaliwa Mara 7 Madrid!
Kylian Mbappe

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, wakiwemo ABC, Maofisa wa klabu hiyo ya La Liga, walifanyia kazi maboresho ya mikataba mara kadhaa katika kuweka masharti ambayo yanaonekana kuvutia zaidi kwa kipaumbele chao cha usajili.

Mkataba wowote ambao Kylian Mbappe angesaini na Real Madrid unatazamiwa kuwa wa angalau miaka sita, huku staa huyu mwenye miaka 22 akitarajia malipo ya €30m (£25.71m kwa msimu, na uwakilishi wake ukinufaika na bonasi ya €60m (£51.43m).

Kwa kuwa bado staa huyu mpaka sasa hajasaini mkataba mpya na PSG, bila shaka Real Madrid wataanzisha jitihada rasmi za kuiwinda saini yake tena mapema mwakani.


BADILI KILA KITU KWA SARAFU MOJA TU!

Unaweza kutengeneza faida kubwa huku ukiwa unaifurahia safari kabambe ya wacheza sarakasi kupitia sloti mpya ya Circus Fever Delux kupitia Kasino ya Meridianbet pekee Dau lako linaweza kukupa pesa maradufu kupitia kete au sarafu.

Uingereza, Sancho Aondolewa Kwenye Kikosi cha Uingereza, Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe