Uwezekano wa kiungo wa Simba, Jonas Mkude kucheza mechi ya kesho dhidi ya Kaizer Chiefs haupo. Si mmoja ya wachezaji waliokuwa kambini tangu waliporejea kutoka Afrika Kusini kucheza mechi ya mzunguko wa kwanza.
Kocha Didier Gomes kwa kumkosa mazoezini Mkude tangu Jumanne, amefanya mipango mingine na nafasi yake anaweza kucheza Mzamiru Yassin.
Mzamiru anaonekana kuandaliwa kucheza sambamba na Thadeo Lwanga , kwani kukosekana kwa Mkude katika awamu tatu za mazoezi maana yake nafasi ya kucheza ni finyu.
Alipoulizwa kocha wa Simba, Gomes alisema:”Mkude amekosekana kambini kutokana na sababu za Kifamilia.” Hakufafanua.
Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.
Magdalena
Duh balaa Sasa ilo
Sarah
Hatari sana
Sauda
Ni shida