Zamani sana dunia ilihitaji fikra za mageuzi, walikuja wanaharakati wengi wenye fikra za kijamaa, wengi hawakuupenda sana ubepari, haikuwa rahisi kuipa dunia sura mpya.
Nageuza dira yake na kumtazama MO Dewji Tajiri kutoka Tanzania anaefanya mengi kwenye klabu ya Simba, ametaka kuleta sura mpya kwenye soka la Tanzania.
Navuta kitabu changu ili nimsome tena Che Guevara Mwanamageuzi kutoka Amerika Kusini, aliwahi kusema “If I move forward, follow me, if I stop, push me and if I go back, kill me“.
CHE aliamini kuleta fikra mpya sio rahisi, kuvunja mizizi ya watu sio rahisi na kuitengeneza dunia mpya sio rahisi, namtazama MO kwenye sura hiyo, bahati mbaya kuna muda anavaa sura hiyo na kuna muda anaivua.
CHE alisema “Akienda mbele watu wamfuate” MO nenda mbele tena na tena kama Che na watu wapo tayari kukufuata ndio maana walikupa NDIO yao, usipende sana kugeuka nyuma.
CHE alisema “Nikisimama Nisukume” basi kubaliana nasi ukisimama tukusukume kama mimi navyokusukuma, achana na hofu, achana na tabia kunguru mwoga anaekimbiza bawa lake.
Lakini CHE alisema “Nikisita basi Mniue” hapa hatuwezi kukuua, nadhani ni fasihi ilitumika nachojua ukisita sisi tutatumia tena wino wetu kukumbusha ulipoitoa Simba, ulipoifikisha na wapi inapaswa kwenda, basi ukisita tukutoe aje mwingine.
Tambua kuwa hakuna kitu chepesi palipo na wengi na demokrasia kwakuwa kila mtu atasema, lakini usisahau “No hurry in Africa” hakuna haraka Afrika tutafika tu, endelea kupambania fikra za mageuzi na tusubiri muda.
MALIZA MWAKA KIBINGWA KWA KUJISHINDIA SHEA YAKO KWENYE SHILINGI 140,000,000TSH!!
Kipindi hiki cha sikukuu kinamalizika kwa namna ya kipekee. Shilingi 140,000,000 kushindaniwa katika michezo ya Evolution kwenye Kasino Mubashara ya Meridanbet. Ingia mchezoni na ujiwekee nafasi ya kushinda shea yako!!!
warda
Maneno mazuri sana nimeyapenda
Rahma
Maneno yako poa sana
Sarah
Nimeyaelewa maneno yako vizuri
Sadick
MO endelea kula mtori nyama utazikuta chini. Mageuzi yoyote hupingwa na mwanamageuzi akikomaa mwisho wake huwa mzuri
Tatu
Maongezi mazuri
Adelta
Mashabiki wanamkubali maongezi kwa sababu ni mazuri
Hopemwaikuka
Changamoto
Issa
Mo dewj bilionea alieibeba simba
Dorophina
Mo haeleweki kama hana msimamo vile na anachotaka kukifanya
Lydia Emmanuel Magoti
Maneno mazuri Sana
Shafii
Gud news
Khadija
Good
Caroline
Uyo ndo che Guevara man
Shakila mrope
Ni changamoto sana
Fatuma kasomo
Maneno mazuri
Magdalena
Jambo zuri
Mwanahamisi
Gud news
Janeflora malisa
Safi
Ester jackson
Habari njema
David Pere
endelea kula mtori nyama utazikuta chini. Mageuzi yoyote hupingwa na mwanamageuzi akikomaa mwisho wake huwa mzuri
aisha
Safi sana