Kiungo fundi anayekipiga katika klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Croatia Luca Modric amesema hafikirii kustaafu soka la kimataifa kwasasa.

Kuelekea mchezo wao dhidi ya timu ya Denmark katiika michuano ya Uefa Nations League nyota huyo amedai hafikirii kustaafu kwasasa kwani anafikiria kuendelea kuiongoza timu hiyo kama nahodha hadi kwenye michuano ya kombe la dunia yatakayofanyika Qatar mwezi wa kumi na moja mwaka huu.

modricKiungo huyo fundi ambae alikuwepo kwenye kikosi hicho wakati kinafika fainali ya michuano ya kombe la dunia miaka minne nyuma na kuonekana kua na ubora uleule wengi waliamini huenda ingekua ndo michuano yake ya mwisho kimataifa mpaka wakati huu akiwa na miaka 37 bado anathibitisha ubora wake.

Modric anaeleza “Sifikirii juu ya hilo sijafanya maamuzi yeyote, Nimeangazia kimataifa zaidi”.

“Tuna nafasi ya kufuzu nne bora kisha tuna kombe la dunia kisha tutaona zaidi”.

“Nitajaribu kufanya uamuzi bora zaidi”,Wakati huo nitajaribu kuongea na kocha wangu pamoja na watu ninaowaamini” Ila sifikirii hilo kwasasa”Alisisitiza Modric.

Modric ameendelea kuonesha nia ya kutaka kulipigania taifa hilo zaidi katika michuano mbalimbali na kusisitiza uamuzi wa kustaafu kwenye timu hiyo ya taifa ni jambo ambalo bado hajalifikiria.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa