Mohamed Salah Amekataa Ofa ya £150M

Mohamed Salah hatarajii kuachana na Mabingwa wa Ulaya Liverpool baada ya kuripotiwa kukataa ofa ya ya paundi miloni 150 zinazotajwa kuandaliwa na Real Madrid na Juventus ili kumnasa Mo Salah.

Toka alipojiunga na wakali hawa mwaka 2017 kwa ada ya paundi 36.9, Mohamed Salah amewafungia Liverpool jumla ya magoli 71 akiwasaidia kwa nafasi kubwa kutwaa ubingwa wa Ulaya msimu uliopita.

Staa huyu alikuwa akihusishwa zaidi na kurejea Italia na kuungana na wakongwe wa La Liga Real Madrid. Lakini yeye ansema kuwa wakati wake wa kusepa klabuni hapo bado. Bado anahitaji mda zaidi klabuni hapobaada ya kupata taji la kwanza na timu hiyo.

Mkataba wa sasa wa Salah unamfanya aendelee kuwepo Liverpool hadi mwaka 2023 ikiwa baada ya kusaini mkataba mpya mwaka uliopita. Hata hivyo anasema kuwa atafikiria hali yake klabuni hapo.

2 Komentara

    Salaha kaon Liverpool ndo mpila wake ulipo akitok t kapotea

    Jibu

    Tena salaha asijaribu kabisa kutoka liverpool ataumbuka na sio kupotea tuu

    Jibu

Acha ujumbe